Waziri Mhagama azindua Programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi wa stadi za maisha ya Taifa kwa vijana mkoani Iringa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Mhe Jenista Mhagama amezindua Programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi wa stadi za maisha ya Taifa kwa vijana, Mkoani Iringa mpango ambao utawanufaisha vijana elfu tatu mianne 3,400 mpango unaogharamiwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli.
Mhe
Mhagama amesema mpango huu ni sehemu ya kuwaandaa vijana ambao watashiriki
katika mapinduzi ya viwanda nchi Tanzania na utasaidia kutoa fursa kwa vijana
kujiajiri na kuajiriwa kupitia mafunzo ya Uanagenzi, katika nyanja za ujenzi,
tehama, ufundi magari, na ushonaji nguo katika mikoa yote nchini Tanzania.
Katika
awamu hii ya kwanza, mpango huu unaendeshwa kwa pamoja baina ya Serikali ya
Tanzania na taasisi ya Wasalesiani wa Don Bosco Tanzania.
Uzinduzi
huo umeshuhudiwa na Naibu waziri Mhe Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Mhe Amina Masenza, Wabunge kutoka mkoa wa Iringa, na Njombe na Mkuu wa Shirika
la Wasalesiani wa Don Bosco Africa Mashariki Fr. Simon Asira.
No comments