SPIKA WA BUNGE APOKEA MSAADA WA MIFUKO 200 YA SEMENTI NA HUNDI YA SH. MILIONI 15 KUTOKA BENKI YA CRDB TAWI LA DODOMA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU, WILAYANI KOGWA, DODOMA.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akipokea hudi ya shilingi milioni 15 na msaada wa Mifuko mia mbili (200) ya sementi kutoka kwa Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi (kushoto) waliotoa ili kusaidia ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Wilayani Kogwa, Dodoma. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akionyesha hudi ya shilingi milioni 15 aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi (kushoto) alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Kogwa, Dodoma kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Ndg. Msafiri Simon.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hudi ya shilingi milioni 15 na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala, Kogwa, Dodoma. Walioshikilia hundi hiyo ni Wanafunzi wa shule hiyo.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Walimu, Wanafunzi wa shule ya Laikala iliyopo Kogwa, Dodoma na wakazi Kata ya Saranga (hawapo pichani), mara baada ya kupokea msaada huo kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi na kulia Diwani wa kata ya Sagara Ndg. Simon Kamando.
No comments