WAJASILIAMALI WAWEZESHWA KUZIKABILI CHANGAMOTO
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeandaa mkakati wa kuwasaidia wajasiriamali nchini kukabiriana na changamoto zinazokwamisha maendeleo yao ili waweze kuchangia juhudi za Serikali katika kujenga uchumi wa viwanda.
Mkurugenzi
wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo ameeleza hivi karibuni kuwa miongoni mwa
mikakati hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa
kushirikiana na taasisi zingine ambazo kwa njia moja au nyingine
zinagusa shughuli za wajasiliamali nchini.
Alizitaja
taasisi hizo kuwa ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la
Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (Tantrade) na GS1, ambazo kwa pamoja zitakuwa zikitoa mafunzo
ya namna ya kuboresha bidhaa za wajasiriamali ili ziendande na mahitaji
ya soko la ndani na nje ya nchi.
“Changamoto
zinazowakabili wajasiriamali ni mtambuka na zinahitaji mikakati ya
pamoja ya sekta na wadau katika kukabiliana nazo”. Alisisitiza Sillo
wakati wa kikao cha pamoja na taasisi hizo.
Ametaja
mkakati mwingine ni kuundwa kwa Kamati ya wataalam nane ambayo
itaratibu namna ya kutekeleza mikakati ya kuondoa changamoto
zinazowakabili wajasiriamali kote nchini. Kamati hiyo itajumuisha
wajumbe wawili kutoka kila taasisi.
Pia
Bw. Sillo amezishauri TanTrade na SIDO kufuatilia katika halmashauri
zote nchini upatikanaji wa maeneo ya uzalishaji yatakayotumiwa na
wajasiriamali hao ili kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda
kwa vitendo.
Kwa
upande wa bidhaa hatarishi (high risk food products), Mkurugenzi wa
TFDA amesisiza bidhaa hizo zisizalishwe bila kuwa na vibali kutoka TFDA
ili kulinda afya ya mlaji na mamlaka hiyo kufanya marejeo ya kanuni ya
ada na tozo ni mkakati wa kuweka unafuu kwa wajasiriamali.
Kuanzia
mwaka 2013/14 hadi 2016/17, TFDA imetoa mafunzo kwa wajasiliamali
katika mikoa 16 ambayo ni Dar es Slaam, Pwani, Mwanza, Arusha, Mbeya,
Dodoma na Rukwa.
Mikoa mingine ni Manyara, Lindi, Mtwara, Tanga, Singida, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro na Morogoro.
Aidha
jumla ya wajasiriamali 1,287 wameisha pewa mafunzo mapaka kufikia mwezi
June, 2017 ambapo kwa sasa mafunzo hayo yatafanyika kwa kushirikisha
taasisi zote zenye jukumu la kuwahudumia wajasiriamali hapa nchini.
No comments