MAMA MAGUFULI ATOA MSAADA KWA VITUO NANE VYA WATOTO YATIMA
Mama Magufuli ametoa msaada huo
leo Jijini hapa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu
vikiwemo vya Newlife, Charambe Islamic Centre, Chakuwama, Mwandaliwa
Yatima Centre, Al Madina Children Home, Alzam Orphanage Centre, Hiari
Orphanage Centre pamoja na Ijangozaidia Orphanage Centre.
Aidha alisema kuwa msaada huo
alioutoa umejumuisha Sukari mifuko 100 yenye jumla ya Kilogramu 2000,
Mchele mifuko 40 yenye jumla ya Kilogramu 2000 pamoja na Tende pakiti
100 zenye jumla ya Kilogramu 800.
“Ninayo furaha kuweza kuwasaidia
zaidi ya watoto yatima 600 ambao wamenuia kufunga katika mwezi huu
Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni muendelezo wa huduma za kujitolea kwa
jamii kwa kuwasaidia watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea Watoto
yatima”, alisema Mama Magufuli.
Mke huyo wa Rais alifafanua kuwa
kituo cha Newlife chenye watoto 121 kimepewa Mchele kilo 363, Sukari
Kilo 363 na Tende Kilo 144, Charambe Islamic Centre chenye Watoto 54
kimepewa Mchele Kilo 162, Sukari Kilo 162 na Tende Kilo 64, Chakuwama
chenye Watoto 64 kimepewa Mchele Kilo 192, Sukari Kilo 192 na Tende Kilo
64 na Al Madina Children Home chenye Watoto 65 kimepewa Mchele Kilo
195, Sukari Kilo 195 na Tende Kilo 64 .
Vituo vingine ni Mwandaliwa
Yatima Centre chenye Watoto 94 kimepewa Mchele Kilo 282, Sukari Kilo 282
na Tende Kilo 64, Alzam Orphanage Centre chenye Watoto 51 kimepewa
Mchele Kilo 153, Sukari Kilo 153 na Tende Kilo 64, Hiari Orphanage
Centre chenye Watoto 41 kimepewa Mchele Kilo 123, Sukari Kilo 123 na
Tende Kilo 40 pamoja na Ijangozaidia Orphanage Centre chenye Watoto 103
kimepewa Mchele Kilo 309, Sukari Kilo 309 na Tende Kilo 104.
Kwa upande wake mwakilishi wa
viongozi wa vituo vya kulelea watoto yatima, Mama Kuluthum Juma alisema
kulea watoto yatima si jambo la mtu mmoja au Serikali peke yake hivyo ni
lazima wananchi wote wajumuike katika kuwasaidia watoto hao kwa hali na
mali ili wajione kuwa wako sawa na Watoto wengine wanaoishi na wazazi
wao.
“Tunamshkuru sana Mke wa Rais,
Mama Janeth Magufuli kwani msaada huu alioutoa kwetu sio mdogo na hakuna
kitu kikubwa kama kutoa sadaka hivyo natoa rai kwa wananchi tujitahidi
kuwasaidia na kuwafariji Watoto hawa kwa sababu ni Watoto wa watu wote
na hakuna aliyependa kuwa hivyo alivyo,” alisema Mama Kuluthumu.
Misaada kwa Watoto yatima na
wanaoishi katika mazingira magumu ni muendelezo wa huduma za kujitolea
kwa Jamii anazofanya Mke wa Rais ambazo hufanyika kila mwaka.
No comments