TIOTE AANGUKA GHAFLA NA KUFARIKI DUNIA AKIWA KWENYE MAZOEZI NI KIUNGO WA IVORY COAST
Kiungo wa zamani wa Newcastle, Cheick Tiote
ameanguka ghafla na kupoteza maisha akiwa mazoezini.
Tiote amepoteza maisha
akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa mazoezini katika kikosi cha Beijing
Enterprises kinachoshiriki ligi daraja la pili.
Kiungo huyo raia wa Ivory Coast amejiunga na
timu hiyo miezi mine tu iliyopita.
Alikimbizwa hospital zikiwa ni juhudi za
kuokoa maisha yake lakini haikuwezekana.
Tiote amewahi kuwa kiungo tegemeo wa timu ya
taifa ya Ivory Coast iliyokuwa inaongozwa na Didier Drogba.
No comments