ARSENAL YAZIPIKU KETE CHELSEA,MAN CITY NA JUVENTUS,YAMNASA BEKI KISIKI WA SCHALKE 04
Arsenal wametangaza kumchukua beki wa kushoto
Sead Kolasinac kutoka Bosnia.
Beki huyo ambaye amekuwa akichezea klabu ya
Schalke ya Ujerumani atajiunga na klabu hiyo majira ya joto.
Mchezaji huyo wa miaka 23, ambaye huchezea
timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina, amejiunga na Arsenal bila kulipiwa pesa
zozote kwa kwua mkataba wake unamalizika katika klabu hiyo.
Atakuwa rasmi mchezaji wa Arsenal Julai 1 soko
la kuhama wachezaji litakapofunguliwa rasmi.
“Beki huyu atajiunga na klabu kwa mazoezi ya
kabla ya msimu Julai,” Arsenal wamesema kupitia taarifa.
Schalke wamethibitisha kwamba beki huyo ametia
saini mkataba Arsenal ambao unadumu hadi 2022.
Klabu hiyo ya Bundesliga imeandika kwenye
Twitter: “Kila la heri siku za usoni na asante sana kwa miaka sita ya fahari.”
Kolasinac aliwasaidia Schalke kumaliza nafasi
ya 10 Bundesliga msimu uliopita na walifika robofainali Europa League ambapo
waliondolewa na Ajax iliyofika hadi fainali.
“Arsenal ina utamaduni wa muda mrefu na
niliifuatilia klabu hii tangu nilipokuwa mvulana mdogo, enzi za Jens Lehmann na
Thierry Henry,” mchezaji huyo aliambia tovuti ya Gunners.
Awali timu kadhaa zilikuwa zikimuwania
Kolasinac wakiwemo mabingwa wa England, Chelsea.
Timu nyingine ambazo zilionyesha nia ya
kumpata kabla ya Wenger kuchangamka ni pamoja na Manchester City, Liverpool,
Everton, Juventus na AC Milan.
No comments