NAKURU TIMU YA TATU TOKA KENYA KUTINGA NUSU FAINALI SPORTPESA SUPER CUP,YAIBUTUA SIMBA YA TANZANIA
Kiungo
wa Simba Mwinyi Kazi Moto (kulia) akiwania mpira na Amani Kyata, wa Nakuru All
Stars, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup,yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
.......................................................................
Mchezo wa pili wa Michuano ya
SportPesa umemalizika kwa Nakuru All Stars kuibuka na ushindi wa jumla ya
Penalti 5-4 mchezo uliomalizika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kwa matokeo hayo timu ya Nakuru
inayocheza Ligi daraja la kwanza nchini Kenya imetinga hatua ya Nusu Fainali
ambapo watakutana na Goria Mahia toka Kenya waliofuzu baada ya kuwafunga
Jang’ombe boys Jumla ya mabao 2-0.
Michuano hiyo itaendelea siku
ya Alhamis kwa mechi mbili kupigwa mchezo wa Mapema utawakutanisha mabingwa wa
Ligi Kuu Tanzania bara Yanga watakaocheza na AFS Leorpads na ya pili itakuwa
kati ya Goria Mahia na Nakuru pia ya Kenya kwa hiyo Kenya wameingiza timu tatu
kwenye Nusu Fainali na bingwa wa Michuano atacheza na Everton ya Uingereza July
13 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Kiungo
wa Simba Mwinyi Kazi Moto (kulia) akiwania mpira na Amani Kyata, wa Nakuru All
Stars, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup,yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
No comments