IGP SIRRO AFANYA ZIARA KIBITI.
IGP Sirro ametuma salamu
hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani humo mara baada ya
kumaliza mazungumzo na wazee wa wilaya ya Kibiti kwa kuwataka wakazi wa eneo
hilo wasiwe na hofu kuhusiana na matukio ya uhalifu yanayoendelea kwa kuwa
yeye mwenyewe ameamua kuingia mzigoni.
Nitume
tu salamu kwao, waendelee tu kukimbia, waendelea kufanya wanayoyafanya lakini
mwisho wa siku tutawarudisha kwenye mstari kwa sababu kikubwa umoja wetu ndiyo
nguvu yetu. Mimi nipo mzigoni nawaomba mtupe muda uchunguzi ufanyike maana
mauaji tokea zamani yapo yanaweza yakawa ya visasi ama namna nyingine kwa hiyo
wana kibiti au wana Rufiji wasije wakaona mauaji mengine ya kawaida
yakawatia mashaka, mauaji toka tunazaliwa yamekuwepo kikubwa ni kwamba watupe
nafasi tuweze kuchunguza tujue ni nini. Wazee wetu wa kibiti wametueleza
taarifa nyingi sana na mnavyojua hawa wahalifu wanaishi ndani ya kibiti, ndani
ya Ikwiriri kwa hiyo wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata
na chanzo cha mambo yote haya“ alisema IGP Sirro
Pamoja
na hayo IGP Sirro amewahakikishia watanzania kuwa kibiti na maeneo mengine ya
Rufiji yapo salama kabisa wala hakuna matishio makubwa kama watu
wanavyoaminishwa.
“Ni wahakikishie watanzania kwa ujumla kibiti na maeneo mengine
ya Rufiji siyo matishio makubwa kama watu wanavyofikiria ni maeneo yanayopitika
watu wanaishi vizuri ni ile hofu iliyokuwepo tumekuja kuangalia hakuna sababu
ya kuwa na hofu hala ni kakundi kadogo kana watu wachache ambao wamebadilika
kuwa shetani sasa dawa ya shetani tunaijua dawa yake , namna ya kumshughulikia
kama shetani” alisisitizia
IGP Sirro
No comments