MTOTO SHUKURU ARUHUSIWA MUHIMBILI , AFYA YAKE YAIMALIKA.
Mtoto
Shukuru Kisonga (16) akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
ambako alifikishwa Mei 16, 2017 kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana
na kusumbuliwa na ugonjwa na Selimundu na upungufu wa madini chuma.
Mtoto huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na
madaktari wa hospitali hiyo.
Mtoto
Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alikuwa amelazwa kutokana na
kusumbuliwa na ugonjwa wa selimundu na upungufu wa madini chuma.
Kushoto ni mama yake Shukuru, Mwanabibi Ntenje
…………………………………………………………………………….
Mtoto
Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) baada ya kupatiwa matibabu na afya yake kuimarika.
Mtoto
Shukuru alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mei 16, mwaka
huu akitokea Tunduru ambako aliripotiwa kuishi kwa kunywa mafuta ,
sukari na maziwa.
Baada
ya kufikishwa MNH alifanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari Bingwa na
kubaini kwamba ana ugonjwa wa Selimundu pamoja na upungufu wa madini ya
chuma na kwamba upungufu wa madini hayo ulisababisha anywe mafuta,
sukari na maziwa.
Kwa
upande wake Mama mzazi wa mtoto Shukuru, Mwanabibi Mtenje amesema
amepata faraja kuona afya ya mtoto wake imeimarika na sasa anaweza kula
chakula chochote.
“Kwakweli
namshukuru Mungu, pia nawashukuru sana madaktari na wauguzi wa
Muhimbili kwani hali ya mwanangu ilikuwa mbaya, alikuwa hawezi kula
chochote zaidi ya kunywa mafuta, maziwa na sukari, lakini baada ya
kupatiwa matibabu, afya yake imeimarika na sasa anaweza kula vyakula
vyote,’’ amesema Mama Shukuru.
Awali
mtoto Shukuru alipelekwa katika Hospitali ya Misheni Tunduru kwa ajili
ya kupatiwa matibabu, lakini ugonjwa haukooneka na baadaye alipelekwa
hospitali Nyangao mkoani Lindi.
No comments