Header Ads

click here

Cheka adai ameonewa kufungiwa miaka 2 na TPBC

Baada ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) wiki iliyopita kutangaza kumfungia miaka miwili Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka kufuatia kitendo chake cha kugoma kupanda ulingoni kupigana na Bondia Abdallah Pazi ‘Dullah’, bondia huyo ameibuka na kudai kuonewa.

Cheka ambaye pia alitangaza kustaafu ngumi wiki hiyo hiyo, amedai mkataba wake na promota Sijaru Kaike ambao ulipelekwa TPBC ulikuwa ni fake.

Mkataba unaodaiwa kuwa fake
Bondia huyo atupia mtandaoni mkataba huo fake na kuandika:



 Ninaposema mkataba umegushiwa namaanisha hivyo hapo chini. Angalieni saini zangu za passport na visa za hivi karibuni, na linganisha na sahihi iliyopo kwenye mkataba wa promota. Je vinaendana?. Na mjue kuwa liliandaliwa pambano na Mthailand mwaka jana na promota huyo Siraju Kaike, mimi nilipewa mkataba wa sh Million 6, baada ya Mechi nikapewa Sh 50,000 tu, sijalipwa deni langu mpaka leo nadai, je wewe kama mshabiki na Mdau wa ngumi ungepanda tena ulingoni bila kupewa hela yako tena?
Na mkataba niliosaini ni kucheza Morogoro, ilikuwa ni ubinadamu kwenda Dar maana Dullah ndio alichotaka, sina mkataba wa PTA, na kama kuvunjika ulianzia hapo.
TPBC mtumie weledi na sio kuwahi kusikika habarini… Na kwa bahati mbaya, mchezo wa Juzi bondia kama Twaha Khassim(Kiduku) mpaka sasa hajalipwa hela yake kamili na huyo Promota Kaike, na ni ndogo sana, Je hiyo yangu ndio angelipa?
Wakuwajibishwa ni nani hapo, Promota au mimi nae onewa?

No comments

Powered by Blogger.