Header Ads

click here

Jay Z na Beyonce waalikwa Ikulu kumuaga Obama By Salum Kaorata on January 5, 2017 - 11:00 am

Jay Z na mke wake Beyonce wamealikwa katika sherehe ya kumuaga Rais Barack Obama Ijumaa hii ya Januari 6.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Ikulu ya Marekani, sherehe hiyo itafanyika kwenye viwanja vya Ikulu hiyo ambapo Rais Obama na mkewe Michelle Obama wanatakuwa washereheshaji.
Mastaa wengine kibao wa nchi hiyo wamealikwa kuhudhuria kwenye sherehe hiyo akiwemo Stevie Wonder, Usher, Oprah Winfrey, Samuel L. Jackson, Bradley Cooper na George Lucas.
Obama anatarajia kumkabidhi rasmi madaraka ya kuiongoza nchi hiyo Donald Trump Januari 20 baada ya kumaliza miaka minane ya uongozi wake

No comments

Powered by Blogger.