Wasanii wasipotafuta elimu nje ya muziki wataendelea kutumika vibaya na watu wenye akili – GK
Kufuatia wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya kuingia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya, rapper mkongwe King Crazy GK amewataka wasanii nchini kutafuta elimu nje ya muziki ili siku mambo yakienda vibaya kwenye muziki wawe na uwezo wa kufanya mambo mengine na kuendesha maisha yako.
Rapper huyo amedai wasanii wengi wanajikuta wamengia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya kukosa mwelekeo katika muziki ambao wanafanya.
“Wasanii wanatakiwa kuitafuta elimu sana kwani wanapaswa kutambua muziki unapanda na kushuka ukiwa na elimu yako muziki hata ukishuka unaweza kwenda kufanya mambo mengine kupitia taaluma yako na ukaendesha maisha yako vizuri,” GK akiliambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Elimu kwa msanii ni kama ‘Life Insurance’ yake usipokuwa na elimu mambo yakiyumba ndiyo wanajikuta wanatumiwa na watu wenye akili zao kufanya mambo ya ajabu ajabu,”
Aliongeza, “Lakini pia wasanii wanatakiwa watambue wao ni kioo cha jamii hivyo wakiwa na elimu ni rahisi kuilisha jamii vitu vizuri kupitia nyimbo zao lakini tukiendelea kuwa na wasanii wajinga wajinga jamii itaendelea kulishwa mambo ya kijinga na kuiharibu jamii yetu”
Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Mzuri pesa’
No comments