Dk. Kigwangalla aagiza TAKUKURU kumkamata Tabibu aliyekula pesa za CHF Butiama
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangalla amemwagiza
mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Butiama mkoani Mara, Saimon
Ngiliule kumsimamisha kazi mara moja Tabibu Danieli Mtatiro wa kituo
cha Afya Kiagata kwa tuhuma za kula pesa za wanakijiji kiasi cha sh.2
milioni zilizotokana na malipo ya mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Pia Dk. Kigwangalla amemwagiza
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU)
kumkamata tabibu huyo ili kuhojiwa na kuchukuliwa hatua. “Nakuagiza
Mkurugenzi msimamishe kazi Bwana Mtatiro na afikishwe TAKUKURU haraka
sana. Huku ni kuujumu mpango wa serikali wa kuwaletea maendeleo kupitia
afya matokeo yake mtu mmoja anachukua pesa za wananchi wanaozipatia
taabu hali inayowafanya wakose matibabu” amesema Dk. Kigwangalla.
Dk. Kigwangalla ambaye yupo katika ziara ya kuimalisha sekta
ya Afya Wilaya za Butiama na Serengeti mkoa wa Mara pia ameweza
kukagua hospitali ya wilaya Butiama pamoja na kuzuru kaburi la Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Nyerere.Dk. Kigwangalla yupo katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili Wilayani Butiama na Serengeti. ambapo anakagua vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali ikiwa katika mpango wa uboresha wa Sekta ya Afya.
No comments