HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI KWA MADEREVA WA KITANZANIA WALIOTEKWA HUKO KONGO NA KIKUNDI CHA WAASI,MAIMAI
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya serikali,wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki BI.MINDI KASIGA amesema kutokana na madereva 24 waliotekwa nyara huko jamuhuri ya kongo na waasi waitwao MAIMAI mwezi uliopita juni 29/2017 na kuachiwa, serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia ubalozi wake uliopo huko kongo imechukua hatua kuweza kuwasilisha rasmi tukio hili kwa serikali ya DRC na kuiomba isaidie kuwaondoa watanzania hao katika eneo hilo hatari kwa ajili ya usalama wao.
Pili mawasiliano ya moja kwa moja na madereva hao yanafanyika ili kujua hali zao na kiwango cha usalama wao kwenye eneo hilo.
Aidha BI.mindi kasiga amesema uongozi wa mgodi wa Namoya umeonesha ushirikiano mkubwa kwa ubalozi ambapo umejulisha hatua zilizochukuliwa ikiwemo kuwahamisha kwa muda wafanyakazi wa mgodi wakiwemo watanzania kwenda katika mji wa kindu jimbo la maniema.
mwisho wizara inawashauri wafanyabiashara na watu wengine wanaokusudia kwenda mashariki mwa DRC kuwa waangalifu au kusitisha kwa muda safari zao kwa kuwa matukio ya kutekwa kwa madereva yamekuwa yakijirudia mara kwa mara.

No comments