GABO ZIGAMBA ATAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA IITWAYO KISOGO..
Msanii wa filamu anaemiliki kampuni ya sarafu media Gabo zigamba leo ametambulisha filamu yake mpya iitwayo kisogo na kuelezea lengo la filamu hiyo.
Pia amesema filamu hiyo imekuja kama mapinduzi katika soko la bongo movie na kwa nia ya kuelimisha jamii kupitia filamu hiyo.
Aidha bwana Gabo zigamba amesema filamu hiyo ya kisogo unaweza ukaipata kwa njia ya simu ya mkononi kwa wale wenye android kwa kupakua app ya uhondo na kujisajili ili kuweza kutizama filamu hiyo ya kisogo.
changamoto kwenye kuandaa filamu amesema zipo ila kikubwa ni kuuvaa uhusika ili kuweza kubeba maudhui ya filamu hiyo ambayo unaindaa na kuifikisha kwa jamii.
No comments