Header Ads

click here

UTURUKI:27 wakamatwa kwa tuhuma za ugaidi Uturuki

27 wakamatwa kwa tuhuma za ugaidi Uturuki
Idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kigaidi mjini Istanbul, nchini Uturuki wakati wa mkesha wa mwaka mpya imefikia watu 27.
Eneo la nje ya klabu ya usiku lilipofanyika tukio la kigaidi siku ya mkesha wa mwaka mpya mjini Istanbul, Uturuki.
Idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kigaidi mjini Istanbul, nchini Uturuki wakati wa mkesha wa mwaka mpya imefikia watu 27.

Polisi wamewakamata watu wengine mjini Izmiya, wakiwemo, mke na mtoto wa mtuhumiwa wa tukio hilo.

Polisi wamesema wamembaini mtuhumiwa, ingawa hawakutaja jina lake na wamesema aliingia nchini Uturuki akitokea nchini Syria.

Mtu huyo alitumia mke na watoto wake kama mwamvuli wa kuingilia Uturuki na mara baada ya kutekeleza shambulio hilo katika klabu ya usiku mjini Istanbul, alikimbia, huku akiwa amesababisha vifo vya watu 38.

No comments

Powered by Blogger.