Header Ads

click here

MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA NA EUROPA LEAGUE YAPIGWA ‘STOP’ KWA MUDA

HATUA zijazo za michuano ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League zimeripotiwa kusogezwa hadi Julai na Agosti kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona linaloendelea duniani kote. 
Mechi zote za timu za taifa zilizopangwa kuchezwa Juni zimeahirishwa ili kuupisha msimu wa 2019-20 ukamilishwe.
Taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) baada ya mkutano uliofanyka kwa video leo. 
Mechi, mashindano na ligi zote za soka Ulaya zimesitishwa tangu katikati ya Machi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, ulioanzia Wuhan huko China mwishoni mwa mwaka jana.

Michuano ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League imesogezwa mbele hadi Julai na Agosti kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona PICHA SOMA ZAIDI  HAPA.

No comments

Powered by Blogger.