ATHARI CORONA YAPOROMOSHA SOKO LA MADINI SHINYANGA
Baadhi ya vikundi vya wachimbaji wadogo wadogo wakiendelea na zoezi la uchenjuaji mchanga wa almasi kwa lengo la kutafuta almasi ndogondogo jana nje kidogo ya mgodi mkubwa wa almasi wa mwadui mkoani shinyanga.
Bw. Makomba Faustine Mchimbaji mdogo wa madini mkoani Shinyanga akiangalia kwa makini kama atafanikiwa kupata almasi wakati zoezi la uchenjuaji wa makinikia ya almasi linaoendelea nje kidogo ya mgodi mkubwa wa almasi wa mwadui mkoani Shinyanga.
Baadhi ya vikundi vya wachimbaji wadogo wadogo wakigombania mchanaga unaodhaniwa kuwa na vipande vya almasi wakati wa zoezi la uchenjuaji mchanga wa almasi kwa lengo la kutafuta almasi ndogondogo jana nje kidogo ya mgodi mkubwa wa almasi wa mwadui mkoani Shinyanga.
... ............ ..................... .......... .........................
..... ......... ........... ....
Bw. Makomba Faustine Mchimbaji mdogo wa madini mkoani Shinyanga akiangalia kwa makini kama atafanikiwa kupata almasi wakati zoezi la uchenjuaji wa makinikia ya almasi linaoendelea nje kidogo ya mgodi mkubwa wa almasi wa mwadui mkoani Shinyanga.
Baadhi ya vikundi vya wachimbaji wadogo wadogo wakigombania mchanaga unaodhaniwa kuwa na vipande vya almasi wakati wa zoezi la uchenjuaji mchanga wa almasi kwa lengo la kutafuta almasi ndogondogo jana nje kidogo ya mgodi mkubwa wa almasi wa mwadui mkoani Shinyanga.
... ............ ..................... .......... .........................
..... ......... ........... ....
Na Anthony Ishengoma- Shinyanga
Athari za mlipuko wa ugonjwa wa Corona maalufu Covid 19 tayari zimeanza kuonekana kutokana na wanunuzi wa madini ya Almasi kutoka vikundi vya wachimbaji wadogo vinavyoendelea na marudio ya makinikia ya mchanga wa almasi kuanza kupungua kwa kasi na wachimbaji hao kushindwa kuuza madini hayo kwa wakati kama ilivyotarajiwa.
Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga SHIREMA Bw. Gregory Kibusi wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya zoezi la uchenjuaji wa makinikia ya almasi linaloendelea katika Kijiji cha Msagala Kata ya Maganzo Wilayani Kishapu nje kidogo ya Mgodi Mkubwa wa Almasi wa Mwadui.
Bw. Kibusi aliongeza kuwa kupungua kwa wanunuzi wa madini hayo kunatokana na wanunuzi wa almasi ndogo ndogo yenye ukubwa wa punje ya sukari kupatikana Nchini India lakini kutokana na Nchi hiyo kukumbwa na ugonjwa wa corona wahindi hawaji tena kununua madini hayo.
Kuhusu malalamiko ya wachimbaji wadogo hao kuhusu ubora wa mchanga huo Bw. Kibusi amesema upatikanaji wa mchanga huo ambao ni takribani tani milioni moja utaendelea kutolewa na mgodi wa Mwadui kwa kuwashirikisha viongozi wa SHIREMA na kuwataka wachimbaji hao kuwa na subira na tayari wamebadilisha mchanga huo baada ya mchanga wa awali kumalizika.
Bw. Kibusi aliongeza kuwa pamoja na changamoto zilizopo tayari makundi sita yanayoundwa na vikundi miamoja tayari yanaendelea na uchenjuaji wa makinia na yanaendelea kupata almasi ndogo ndogo na tayari wamekusanya vipande vya almasi takribani 630 na kutokana na zoezi hilo kuendelea wanatarajia kuendelea kupata vipande zaidi vya almasi.
Naye Afisa Madini Mkoa wa Shinyanga Bw. Bariki Munuo Afisa Madini Mkoa wa Shinyanga aliongeza kuwa wachimbaji wanapata madini lakini yanaifadhiwa na ofisi ya madini mkoa kutokana na madalali wa madini kukosa mitaji jambo ambalo linachangiwa janga la corona.
Aidha Afisa huyo wa madini aliongeza kuwa kiwango cha madini hayo ni kidogo kwa kuwa kikundi kinaweza kuchenjua kiwango kikubwa cha mchanga na kupata kipande kidogo sana cha almasi na wakati mwingine kukosa kabisa na changamoto nyingine wanapofanikiwa kupata mzigo unawekwa ndani wasijue ni lini watafanikiwa kuuza kutokana na ufadhili wa watu wanje kupunguza ufadhili kwa madalali wa madini.
Bw. Simon Malila ambaye ni mchenjuaji wa makinikia ya almasi amepongeza mpango wa Serikali kufanikisha zoezi hilo lakini pia hakusita kuomba kupatiwa mchanga unafaa zaidi na kudai kuwa mapato yatakayopatikana kutokana zoezi hilo yatasaidia kuinua kipato cha familia.
No comments