Header Ads

click here

NGASSA AJIFUA KIVYAKE KWA UCHUNGU

KUFUATIA kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Mrisho Ngassa, mipango yake ya kutaka kurudi Yanga kugonga mwamba, nyota huyo ameamua kujifua vikali jijini Mwanza ili kurejesha kasi yake kama zamani.

Ngassa ambaye alijiunga na Mbeya City kwenye dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Fanja ya Oman, alikuwa na wakati mgumu kwenye kikosi hicho, ambapo tangu alipojiunga nacho, hakuwa na mwendelezo wa kupachika mabao kama ilivyokuwa zamani alipozitumikia Simba, Yanga na Azam FC. Hivi karibuni, Ngassa alitaka kuichezea Yanga kwenye michuano ya SportPesa Super Cup, lakini alishindwa kutokana na kigogo mmoja wa Yanga kumzuia.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ngassa ameweka bayana kuwa, kwa sasa ana hasira sana na soka la Bongo kutokana na watu kuendelea kubeza kiwango chake kwamba kimeshuka, hivyo anataka kuwaziba midomo.
“Dah, ndugu yangu acha nijifue tu ili niweze kuwaonyesha msimu ujao, ujue watu wanaongea mambo mengi sana juu yangu na kubwa ninaumia mno, nikisikia eti wanasema nimeisha wakati hata kwenye ligi hii hakuna mwenye uwezo wa kutisha kiasi cha kufikia hata rekodi yangu
.
“Nipo Mwanza sasa najifua vikali, lengo ni kujiweka fiti ili tutakapoanza mzunguko ujao niweze kuwakimbiza hadi wachoke, sihitaji kabisa mzaha na mtu yeyote msimu ujao na wala sitakuwa na urafiki na timu wala mtu, zaidi wajipange kuona ninawatesa uwanjani


No comments

Powered by Blogger.