Header Ads

click here

Ijue michuano ya mataifa ya Africa (AFCON)

dfffd
AFCON ni kifupi cha Africa Cup of Nation haya ni mashindano yahusuyo mataifa ya Africa ambayo ni mwanachama wa CAF,AFCON ilianza rasmi mnamo mwaka 1957 na kuanzia mwaka 1968 mashindank haya yalianza kufanyika kila baada ya miaka miwili.
Mwaka 1957 mashindano haya yalihusisha timu tatu tu ambazo ilikuwa ni Egypt,Sudan na Ethiopia kuanzia hapo mataifa yaliongezeka kwani kufikia mwaka 1998 kulikuwa na mataifa 16 katika mashindano yaliyofanyika nchini Burkina Fasso huku Nigeria wakijitoa katika mashindano hayo na idadi ya timu kubaki 15.Lakini kuanzia hapo hadi sasa AFCON imekuwa ikihusisha mataifa 16.
Misri ndio taifa linaloongoza kuchukua kombe hilo kwa kulichukua mara 7 tangia kipindi nchi hiyo ilipokua ikijulikana kama United Arab Republic,kuanzia miaka ya 2000 Mafarao walizidi kuleta utawala wao katila mashindano haya na mwaka 2010 nchini Angola Mafarao waliweka rekodi ya kuchukua kombe hilo mara 3 mfululizo baada ya kuwafunga Ghana kwa goli 1 kwa bila wakawa taifa la kwanza kuchukua kombe hilo mara 3 wakiungana na nchi za Argentina,Mexico na Iran ambao nao wameweza kufanya hivyo katika mashindano yao.
Samuel Etoo mshambuliaji wa zamani wa Cameroon ndiye anashikilia rekodi ya mfungaji magoli mengi katika AFCON akiwa ameweka kambani idadi ya magoli 18 katika mashindano yote aliyoshiriki na timu yake ya taifa akifuatiwa na mchezaji wa zamani wa Ivory Coast Laurent Pokou na magoli yake 14.
Wachezaji Rigobert Song na Ahmed Hassan ndio wachezaji ambao wamewahi kushiriki michuano hii mara nyingi zaidi huku kila mmoja akiwa ameshiriki mara 8 wakati mataifa ya Misri na Ghana wenyewe wameandaa michuano hii mara nyingi zaidi kila mmoja akiwa ameiandaa mara 4.Tanzania ilishawahi kufuzu kucheza AFCON pale Lagos Nigeria mnamo mwaka 1980 lakini yapo mataifa kama vile Eritrea,Djibouti,Gambia,Lesotho,South Sudan,Somalia,Comoro,Mauritania, Madagascar na Burundi hawajawahi kufudhu kushiriki AFCON.
Mwaka huu kwa mara ya 31 AFCON inaenda kuchezwa nchini Gabon ambapo mshindi atafuzu kucheza mashindano ya Fifa Confederation Cup nchini Russia mwaka huu baadae timu zitakazoshiriki ni Gabon,Morocco,Algeria,Cameroon,Senegal,Egypt,Ghana,Guinea Bissau,Zimbabwe,Mali,Ivory Coast,Uganda,Burkina Fasso,Tunisia,DR Congo na Togo.

AFCON tangu ianzishwe ina kikosi bora ksbisa cha muda wote kinachoundwa na Kipa:-Essam El Hadarry,Mabeki:-Geremi Njitap,Kolo Toure,Sammuel Kuffour na Taye Taiwo,Viungo:+Mohamed Aboutrika,Yaya Toure,Michael Essien na Jay Jay Okocha huku washambuliaji ni Samuel Etoo na Didier Drogba.

No comments

Powered by Blogger.